Mwakilishi wa wadi ya Mkomani kaunti ya Lamu Shekhuna Abbas amesisitiza kuwa ukuzaji wa talanta na vipawa miongoni mwa vijana utasaidia pakubwa kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya.
Abbas amesema ili kuafikia swala hilo ni sharti kuwe na ushirikiano baina ya viongozi na wakaazi wa eneo hilo.
Mwakilishi wa wadi huyo pia amesema ukosefu wa ajira umesababisha idadi kubwa ya vijana kujihusisha na utumizi wa mihadarati.
Akiunga mkono kauli hiyo mwakilishi wa wadi mteule Ahmed Medo amesema bunge la kaunti hiyo ya Lamu liko tayari kupitisha miswada ya kukuza na kuboresha talanta za vijana katika kaunti hiyo ili kuwaimarisha pakubwa.
SHEKHUNA ABBAS ASEMA UKUZAJI WA TALANTA KAUNTI YA LAMU

