JAMII WA WABAJUNI KAUNTI YA MOMBASA WAMPONGEZA GAVANA ABDULSWAMAD SHARIFF NASSIR

Siku chache baada ya gavana wa kaunti ya Mombasa Abdhulswamad Shariff Nassir kutangaza baraza lake la mawaziri, jamii ya wabajuni katika kaunti hiyo imempongeza Gavana huyo kwa kumteua Daktari Mbwarali Kame Mborali kama waziri wa elimu wa elimu na masuala ya kidigitali.
Wakiongozwa na mzee wa jamii hiyo kaunti ya Mombasa Omar Shariff, wanasema wako tayari kufanya kazi kwa karibu na gavana Nassir kwa lengo la kuhakikisha ajenda zote za serikali yake zinafaulu katika kaunti hiyo.
Kwa upande wake sheikh Abu Hamza ambaye pia ni mmoja wa jamii hiyo amemshukuru gavana Nassir na kuwataka mawaziri wote kwenye kaunti hiyo kushirikiana katika kuwahudumia wenyeji.