ALI MBOGO AWATAKA WENYEJI WA MOMBASA KUWA NA SUBIRA

Aliyekuwa mbunge wa Kisauni Ali Mbogo ametoa wito kwa wenyeji wa kaunti ya Mombasa kuwapa muda viongozi waliochaguliwa kwenye kipute cha Agosti 9 mwaka jana wa 2022 ili kuwahudumia.
Mbogo ambaye alikuwa akizungumza kwenye mtaa wa Bilima eneo bunge la Kisauni kaunti ya Mombasa amesema bado ni mapema kuwalaumu viongozi hao kwa utendakazi duni na kusisitiza haja ya kupewa muda zaidi.
Kulingana na Mbogo iwapo viongozi hao watapewa muda mzuri huenda wakatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuwafanyia wenyeji miradi ya maendeleo.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na baadhi ya vijana katika eneo hilo la Bilima wakidai kukosa kupewa nafasi za ajira kwenye mpango wa kazi ambao uliidhinishwa kwenye kaunti ya Mombasa hata baada ya kutuma maombi ili kuajiriwa.