Aliyekuwa gavana wa kwanza wa kaunti ya Taita Taveta John Mruttu amesema mzozo kuhusiana na mipaka kati ya kaunti hiyo na zile zinazopakana na Taita Taveta utapata mwafaka kupitia sheria na sio mivutano.
Mruttu amesema migogoro hiyo inakumba mipaka ya kaunti ya Taita Taveta, Kajiado, Kwale na Makueni itapata mwafaka iwapo viongozi wa kaunti hizo watafuata sheria pekee.
Amesema iwapo wanasiasa wataendelea kurushiana cheche za maneno hakutawahi kupatikana mwafaka wa mzozo huo.
Kwa sasa ametaka jopo ambalo aliliunda alipokuwa gavana wa kaunti ya Taita Taveta kushughulikia mzozo huo ili kumaliza migogoro hiyo.
JOHN MRUTTU ASEMA MZOZO KUHUSU MIPAKA KATI YA KAUNTI YA TAITA TAVETA NA ZILE ZINAZOPAKANA NA KAUNTI HIYO UNAPASWA KUTATULIWA KISHERIA

