SERIKALI NA MASHIRIKA MBALIMBALI YATAKIWA KUSAIDIA KATIKA KUTOA CHAKULA CHA MSAADA KAUNTI YA TANA RIVER

Mkurugenzi wa shirika la Msalaba mwekundu kaunti ya Tana River Gerald Bombe ametoa wito kwa mashirika mbalimbali pamoja na serikali kusaidia katika kutoa chakula cha msaada kwa wananchi ambao wanaendelea kuathirika na baa la njaa nchini.
Bombe amesema zaidi ya wenyeji laki moja katika kaunti ya Tana River waliathirika na baa la njaa kufikia mwishoni mwa mwaka jana wa 2022.
Amesema eneo la Tana Kaskazini ndilo ambalo liliathirika zaidi katika kaunti ya Tana River.

Wakati huohuo amehimiza kuendelezwa kwa mpango wa kununua na kuchinja mifugo licha ya kumalizika kwa idadi ya mifugo iliyokuwa inalengwa na serikali.