Mwenyekiti wa baraza kuu la ushauri kwa Waislamu nchini KEMNAC Sheikh Juma Ngao ametoa wito kwa serikali kuingilia kati madai kuwa abiria wanaokabiliwa na dharura na kushindwa kusafiri kuwa hawawezi kurudishiwa nauli zao na usimamizi wa shirika la reli ya kisasa la SGR.
Sheikh Juma Ngao amesema baadhi ya abiria wamekuwa wakilalamikia hilo na kuitaja kanuni hiyo ni sawa na ulaghai hali ambayo amesema inapaswa kutafutiwa mwafaka.
Amesema imekuwa vigumu kwa abiria kuregeshewa fedha zao kila panapotokea dharura.
SHEIKH JUMA NGAO AITAKA SERIKALI KUINGILIA KATI NA KUTATUA LALAMA ZINAZOIBULIWA KUHUSU SGR

