Mbunge wa Matuga kaunti ya Kwale, Kassim Sawa Tandaza amekosoa hali ya kucheleweshwa kwa malipo ya baadhi ya wanakandarasi wanaotekeleza kandarasi ambazo wanapewa na serikali ya kitaifa.
Tandaza ambaye alikuwa akizungumza bungeni alipokuwa akiunga mkono sheria ya usimamizi wa fedha za umma, ametaka mradi wa Dongo Kundu ambao umebakisha asilimia 6 kukamilika ila mwanakandarasi hajalipwa fedha zake.
Ameitaka serikali kuharakisha na kukamilisha fedha hizo ili mradi huo ukamilishwe kama ulivyokuwa umeratibiwa.
Aidha, amesema iwapo mwanakandarasi anapocheleweshewa malipo yake, hali hiyo husababisha riba kupanda na kufanya deni kuongezeka.
KASSIM SAWA TANDAZA AKOSOA HALI YA KUCHELEWESHWA KWA MALIPO YA WANAKANDARASI KAUNTI YA KWALE

