WANAHARAKATI WA KIKE KAUNTI YA LAMU WALALAMIKA

Baadhi ya wanaharakati wa kike kaunti ya Lamu wametoa wito kwa asasi za usalama kufunga maeneo yote ya Mangwe za pombe ya mnazi ambazo ziko kwenye kaunti hiyo.
Kulingana na wanaharakati hao wakiongozwa na Virginia Wangui wamesema kutokana na ongezeko la sehemu hizo za Mangwe maeneo ya Hindi na Mpeketoni, watoto wengi wenye umri mdogo wameanza kuwa waraibu wa pombe hiyo ya Mnazi.
Wanaharakati hao wamesema vijana wamekuwa wakijusisha na visa vya wizi wa Kuku na Mbuzi ili kupata fedha za kununua pombe ya Mnazi.
Ametoa wito kwa Mahakama kuwakabili kisheria vijana ambao wanajihusisha na wizi kufungwa kifungo cha zaidi ya miaka minne kama funzo kwa wengine ambao wanajihusisha na visa hivyo.