WANAWAKE WAJAWAZITO KAUNTI YA KILIFI WAHIMIZWA KUJUA HALI ZAO ZA AFYA PAMOJA NA ZA WAUME ZAO

Afisa wa ushauri kwa wagonjwa ambao wameambukizwa virusi vya ukimwi kwenye hospitali ya Gede kaunti ya Kilifi, Mary Teresia amewahimiza wanawake kaunti ya Kilifi kujua hali zao za afya pamoja na za waume zao wanapohudhuria kliniki wanapokuwa wajawazito.
Teresia amesema hatua hiyo itachangia kupunguza visa vya maambukizi hayo kutoka kwa mama hadi mtoto wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa Mary Teresia amesema wanawake wajawazito walio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi wanapaswa kuhudhuria Kliniki ili kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi hayo.
Vilevile, amesema idadi ya visa vya maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama hadi mtoto vimepungua kutokana na huduma ambazo zinatolewa ili kuwalinda watoto hao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *