Mkuu wa kituo cha Polisi cha Hindi kaunti ya Lamu Sammy Kamwara ametoa onyo kwa wazazi katika eneo hilo dhidi ya kuwapa vijana pikipiki ambao hawana vibali hitajika kwa mujibu wa sheria za barabarani na watakaopatikana watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Kamwara amesema kumekuwa na ongezeko la ajali katika eneo la Hindi kutokana idadi kubwa ya vijana wadogo wasiofahamu sheria za barabarani ambao wamekuwa wakichangia kwa visa hivyo kushuhudiwa.
Amesema wazazi kwenye eneo hilo wamekuwa wakiwapa pikipiki hizo bila kujali iwapo watahusika kwenye visa vya ajali za barabarani au la.
WAZAZI ENEO LA HINDI KAUNTI YA LAMU WAONYWA
