GAVANA ABDULSWAMAD SHARIFF NASSIR AWATAKA VIONGOZI WA KAUNTI HIYO KUWEKA KANDO TOFAUTI ZAO ZA KISIASA

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir amewataka viongozi kuzika tofauti zao za kisiasa na kushirikiana kwa manufaa ya kizazi cha baadae.
Gavana huyo amewataka kuendelea kuhubiri amani na umoja, kila wanapopanda kwenye majukwaa na kukoma kuleta migawanyiko, ambayo baadae huleta mihemko na hatimaye wengine kuchuku hatua zisizo na manufaa kwa jamii
Kwa upande wake Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro, amewapongeza wenyeji kwa kumpa fursa ya kuwa Gavana wa kaunti ya Kilifi na kuahidi kufanyia kila mmoja kazi bila ubaguzi wowote.
Vile vile amewataka viongozi walioko kwenye vyama vingine, kumuunga mkono na kufanya naye kazi muda huu, anapotawala kwa manufaa ya jamii ya wana Kilifi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *