Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi anatarajiwa kumwakilisha rais William Ruto kwenye mkutano muhimu nchini Uingereza kuanzia hii leo.
Kulingana na afisi yake Mudavadi ameondoka nchini hapo jana akielekea Uingereza kuhudhuria mkutano wa kibiashara la mataifa wanachama wa jumuiya ya madola yani common wealth trade and investment summit.
Ni mkutano ulioandaliwa na baraza la kibiashara la jumuiya ya madola, kongamano la kibiashara la jumuiya ya madola linatarajiwa kufanyika kati ya leo na kesho ambalo linafuatia lililofanyika nchini Rwanda, Kigali mwezi juni.
Kwenye taarifa nyingine Mudavadi amelalamikia kuwepo kwa mshindani wa chama cha UDA katika kipute cha useneta kaunti ya Bungoma.
Akizungumza katika kampeni za kumpigia debe mwaniaji wa chama cha Ford Kenya Wafula Wakoli Mudavadi amekariri kuwa kulikuwa na maafikiano ya kukiachia chama cha Ford Kenya wadhfa huo japo baadhi ya viongozi wamekiuka maafikiano hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *