Kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga ameshikilia kuwa jumatano ya wiki hii itakuwa siku ya kuweka wazi mambo yaliyofanyika katika uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu.
Akizungumza katika mtaa wa utawala kwenye kampeni za chaguzi ndogo za uwakilishi wadi, Raila amehoji kuwa ni sharti serikali ya Kenya kwanza iwekewe vidhibiti.
Raila amesema kuwa rais William Ruto anaonyesha dalili za uongozi wa kiimla hivyo asipodhibitiwa taifa hili litaendeshwa kidikteta.
Kinara huyo wa azimio ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwatetea makamishna wanne wa IEBC waliosimamishwa kazi amewataka wakenya kujitokeza kwa wingi jumatano hii kwenye uwanja wa kamukunji ili wajadili maswala mengi yanayolikumba taifa.
Raila ameashiria kuwa kuanzia siku hiyo ya jumatano kuna uwezekano wa kuanzishwa rasmi kwa maandamano ambayo hayatakoma hadi pale kutakapokuwa na mageuzi ya kiuongozi.
Wakati uo huo Raila amepinga madai kuwa azimio la umoja imesambaratika na badala yake amesema kuwa wako imara kubadilisha uongozi wa taifa hili.
RAILA ODINGA ANGALI ANASHIKILIA MSIMAMO WAKE WA KUANDAA MAANDAMANO
