Viongozi wa muungano wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Pwani mjini Kilifi kaunti ya Kilifi, wamelalamikia ukosefu wa usalama ndani ya chuo hicho na katika baadhi ya maeneo ya mjini Kilifi.
Kulingana na viongozi hao wakiongozwa na Kelvin Nyambura pamoja na Riziki Mohammed Yusuf anayehusika na masuala ya jinsia na maslahi ya wanafunzi katika chuo hicho, wamedai idadi kubwa ya wanafunzi wamekuwa wakivamiwa na hata kupokonywa simu na vipakatalishi vyao.
Wakizungumza na wanahabari wamesema hali hiyo ya ukosefu wa usalama pamoja na visa vya dhuluma za kinjia hasa kwa wanafunzi wa kike katika taasisi hiyo, vimeathiri pakubwa shughuli za masomo ya wanafunzi hao.
Aidha, wanatoa wito kwa wizara ya usalama nchini, kuangazia zaidi suala la kujenga kituo cha polisi katika chuo hicho.
VIONGOZI WA MUUNGANO WA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA PWANI WALALAMIKIA UKOSEFU WA USALAMA

