MIKAKATI YA KUTOSHA YA MAANDALIZI YA MTIHANI WA KITAIFA YAWEKWA TANA RIVER

Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Tana River Khalif Hassan amesema mikakati ya kutosha imeweka kuhakikisha matayarisho ya kuandaliwa kwa mtihani wa kitaifa yanaendelea vyema bila changamoto zozote.
Amesema jumla ya wanafunzi 17,166 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kitaifa kwenye kaunti hiyo wakiwemo wale wa darasa la 6 ambao watakuwa wanajiunga na shule za upili mwaka ujao wa 2023 kulingana na mtaala mpya wa elimu wa umilisi CBC.
Kulingana na Hassan licha ya kuwa kunashuhudiwa mvua kwenye maeneo mbalimbali katika kaunti hiyo, baraza kuu la mitihani nchini KNEC limeweka mikakati thabiti kuhakikisha inaandaliwa katika mazingira bora.
Vilevile, amesema mwaka huu hakutakuwa na utaratibu wa kuchanganya watahiniwa kutoka shule mbalimbali ili kufanyia mitihani yao kwenye shule moja.