Kamishna wa kaunti ya Mombasa John Otieno amesema wamefanikiwa kumnasa mmoja wa washukiwa wa visa vya uvamizi katika eneo bunge la Kisauni.
Kulingana na kamishna huyo mshukiwa huyo ambaye ni miongoni mwa wale ambao wanahusishwa na visa vya uvamizi ambavyo viliripotiwa kwenye eneo bunge hilo siku chache zilizopita, alinaswa kufuatia ushirikiano baina ya wenyeji na asasi za usalama.
Amesema mshukiwa huyo ni sugu kwani ripoti za polisi zinaonyesha kuwa aliwahi kutumikia kifungo cha jela kutokana na makosa ya kuvamia wenyeji.
Kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa na maafisa wa polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kukamilishwa kwa uchunguzi dhidi yake huku juhudi za kumsaka mwenzake zikiendelezwa na asasi za usalama.
MSHUKIWA MMOJA WA VISA VYA UVAMIZI ENEO LA KISAUNI ATIWA MBARONI

