Mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu katika shirika la kutete haki za kibinadamu la HURIA kaunti ya Mombasa Alex Nziwi ametoa wito kwa umma kuwaripoti washukiwa wa wizi na sio kuchukua sheria mkononi.
Nziwa ambaye alikuwa akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu amekosoa hatua ya wananchi kuwapiga washukiwa wa uhalifu au hata kuwaua akisema ni ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Aidha, amesema ni wajibu wa asasi za usalama na idara ya mahakama kuwakabili kisheria ili wanaopatikana na hatia washtakiwe na kufunguliwa mashtaka iwapo watapatikana na hatia.
Wakati uo huo, amewataka wananchi kutoa ushahidi mahakamani kwani washukiwa hao huachiliwa huru endapo ushahidi wa kutosha hautapatikana.
WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUWARIPOTI WAHALIFU KWA ASASI HUSIKA

