Familia moja eneo la Kakoneni wadi ya Jilore kaunti ya Kilifi imepatwa na mshangaa kufuatia tukio la ng’ombe wao kuzaa ndama aliyekuwa na viungo kama vya binadamu.
Akiongea na Lulu fm, Bendera Kabaya ambaye ni mmiliki wa ng’ombe huyo amesema kuwa tukio hilo limewastaajabisha wao na hadi majirani kwani ni tukio lisilokuwa la kawaida.
Kulingana na Bendera huenda ikawa mbinu za kishirikina zilitumika kusababishia ng’ombe huyo kuzaa ndama mwenye viungo vya binadamu badala ya mnyama.
James Kazungu Chai ambaye ni mwanawe mama Bendera amesema kuwa tukio geni ambalo hawajawahi kulishuhudia hasa kwa mifugo wao akihoji kuwa ndama huyo alizaliwa tayari akiwa amekufa.
Hatahivyo afisa wa mifugo hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Godrick Mwaringa amesema kuwa ni hali ya kawaida inayopata baadhi ya mifugo akipinga swala kuwa huenda ikawa ni ushirikina uliosababisha ng’ombe huyo kuzaa ndama mwenye mwonekano wa binadamu.
KIHOJA CHAZUKA KAKONENI BAADA YA NG’OMBE KUZAA NDAMA MWENYE SURA YA BINADAMU

