Viongozi mbalimbali eneo la Mariakani eneo bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi wanatoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kilifi kufutilia mbali leseni za wafanyabiashara wa vyuma chakavu.
Wakiongozwa na aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Mariakani Francis Kimosho wanadai kuwa wizi wa vyuma umekithiri eneo hilo licha ya serikali kuu kupiga marufuku biashara hiyo.
Ameitaja hatua hiyo kuchangia kwa uharibifu mkubwa wa miundo msingi eneo hilo.
Naye meneja wa mji wa Mariakani Mary Gituka ameahidi kushirikiana na wadau husika ili kutatua changamoto hiyo ambayo wanadai kuendelea kuwaathiri wenyeji.
WIZI WA VYUMA CHAKAVU UMEKITHIRI ENEO LA KALOLENI KAUNTI YA KILIFI

