MIKAKATI YAWEKWA NA SERIKALI YA LAMU KUDHIBITI WIZI WA MADAWA KWENYE VITUO VYA AFYA

Serikali ya kaunti ya Lamu inalenga kutumia mfumo wa kidijitali katika vituo vya afya ili kupunguza wizi wa dawa.
Gavana wa kaunti hiyo Issa Abdallah Timammy amesema wizi wa dawa umekuwa changamoto kubwa inayokabili idara ya afya kaunti hiyo hali inayodunisha utoaji huduma bora za afya katika kaunti hiyo.
Gavana Timammy amesema kuwa mpango huo wa kidijitali unasaidia kuweka uwazi sawia na kuwafichua maafisa wanaoendeleza ufisadi katika swala la ununuzi wa dawa kwenye kaunti hiyo.
Timammy amesema kuwa serikali yake kwa sasa imewekeza shilingi milioni nne kwa mpango wa kununua vifaa vya kidijitali vitakavyotumika kwenye vituo vya afya.