Afisa wa mipango katika shirika la umoja wa mataifa la chakula ulimwenguni FAO, katika kaunti ya Taita Taveta Abedi Mbatha ameishauri jamii kuendekeza kilimo cha bustani katika makazi yao kama mbinu mojawapo ya kuimarisha uzalishaji wa chakula.
Mbatha amesema kuwa iwapo kila jamii itaanzisha mfumo wa kilimo cha bustani majumbani mwao ni wazi kuwa kiwango cha chakula kitaongezeka majumani na jamii kwa jumla.
Mbatha ,amesema wakaazi wale wanaoishi mijini ambao hukumbwa na uhaba wa ardhi ya kufanya kilimo wanapaswa pia kushiriki katika kilimo cha kutumia magunia ili kuzalisha chakula cha kutosha kilicho na virutubisho hitajika jambo litakalopunguza uhaba wa chakula mijini.
JAMII TAITA TAVETA YASHAURIWA KUANZISHA MFUMO WA KILIMO CHA BUSTANI

