Kamishna wa kaunti ya Taita Taveta Loyford Kibaara amesema kuwa wanatarajia kuanza kupokea chakula cha msaada kutoka kwa serikali kuu.
Amesema chakula hicho kitakabidhiwa wale ambao wameathirika na baa la njaa katika kaunti hiyo.
Akizungumza katika kaunti hiyo amezitaka kamati ambazo zitashughulikia ugavi wa chakula hicho kukakikisha kinapewa walengwa bila kumbagua yeyote.
Aidha, amesema viongozi katika kaunti hiyo wanaendeleza juhudi kuhakikisha wenyeji wa kaunti ya Taita Taveta wanapata chakula cha msaada ili kukabili hali hiyo ya baa la njaa.
Akizungumzia suala hilo la Ukame gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime amethibitisha kuwa wamepokea magunia 400 ya mchele na 150 ya maharagwe ili kuwasaidia wale ambao wameathirika na baa la njaa kutokana na kiangazi ambacho kimekuwa kikishuhudiwa kwa muda mrefu.
Ni msaada ambao umetoka kwa serikali kuu na kuwahimiza wahisani mbalimbali kujitokeza ili kuwasaidia wenyeji wa kaunti hiyo ambao wanakabiliwa na hali hiyo.
KAMISHNA WA TAITA TAVETA ASEMA WANATARAJIA KUPOKEA MSAADA WA CHAKULA

