Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amesema tayari serikali kuu imewasilisha chakula cha msaada kwa wenyeji ambao wanaendelea kukabiliwa na baa la njaa.
Fatuma amesema chakula hicho kitasaidia kwa kiasi Fulani kudhibiti baa hilo, mikakati kabambe inapoendelea kuwekwa na serikali ya kaunti ili kutatua hali hiyo.
Gavana huyo amesema wanaendeleza ujenzi wa mabwawa mbalimbali ili kutatua changamoto ya ukosefu wa maji ambao umekuwa ukishuhudiwa mara kwa mara.
Kauli yake imeungwa mkono na kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi ambaye amewahimiza viongozi wa kaunti na wale walioko kwenye serikali kuu kushirikiana ili kuikabili hali hiyo ya Ukame na baa la njaa kaunti ya Kwale.
Wawili hao wamewasihi wawekezaji kuzingatia sheria kuhusiana na umiliki wa ardhi kabla ya kuwafurusha wenyeji.

