Mwakilishi wa wadi ya Sokoke kaunti ya Kilifi Thaura Mweni, anadai gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro alitumia upendeleo katika kuwateua mawaziri katika baraza lake la mawaziri.
Mweni anadai eneo bunge la Ganze, lilitengwa na halikupata nafasi hata moja ya uwaziri, akidai waziri aliyeteuliwa kushikilia idara ya majanga Felkin Kaingu sio mkazi wa Ganze .
Amesema kila eneo bunge kaunti ya Kilifi lilipaswa kupatiwa nafasi ili liweze kuwakilishwa vizuri katika serikali ya kaunti ya Kilifi.
Kwa upande wake waziri mteule wa utumishi wa umma, mipangilio maalum pamoja na majanga kaunti ya Kilifi Felkin Kaingu, amekanusha madai hayo akisema yeye ni mkazi wa Ganze na kuwataka wanasiasa kushirikiana ili waweze kuwafanyia kazi wakazi wa Kilifi.
GIDEON MUNG’ARO ALAUMIWA KWENYE UTEUZI WA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

