Himizo linazidi kutolewa kwa wanandoa kutatua mizozo yao kwa njia inayofaa ili kudhibiti visa vya mauaji kati yao.
Haya yanajiri baada ya watoto wawili kuzikwa jana kufuatia kuuliwa na baba yao juma moja lililopita huko Bombolulu eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa.
Watoto hao Daniel Jackson Chacha mwenye umri wa miaka minane na David Boke Jackson wa miaka minne walikumbana na kifo chao wiki jana baada ya mzozo kuzuka baina ya wazazi wao hali iliyomlazimu mama yao
Maria Boke kukimbilia usalama wa maisha yake na kuwaacha na baba yao Jackson Chacha.
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa maiti ya watoto hao iliyofanyiwa katika hospitali kuu ya kanda ya pwani ilibaini kuwa wawili hao walinyongwa na kisha miili yao kuteketezwa kwa moto.
Baba ya watoto hao naye alijiua akiwa kaunti ya Taita Taveta baada ya kutekeleza mauaji hayo
WANANDOA WAHIMIZWA KUTOWADHURU WATOTO WAO

