Baadhi ya wazazi wa Garsen kaunti ya Tana River wamewahimiza vijana kujiepusha na mizozo ili kudhibiti visa vya watu kuuwana kwenye ndoa na kuwataka kutatua migogoro baina yao kwa njia inayofaa.
Wamesema ndoa nyingi zinakosa kudumu, kutokana kile ambacho wanadai kuchangiwa na visa vya ulevi na pia wanandoa kuchunguzana hali inayochangiwa na kutokuaminiana kwenye ndoa.
Wamewataka vijana kuhakikisha wanafanya maamuzi ya busara, kwa kuzichunguza tabia na mienendo kabla ya kuoana.
Vilevile, wamewahimiza wanandoa kuheshimiana na wanawake kuwa wanyenyekevu na kuwataka wanaume kujiepusha na mipango ya kando ili kulinda ndoa zao.
VIJANA KAUNTI YA TANA RIVER WAHIMIZWA KULINDA NDOA ZAO

