Serikali ya kaunti ya Mombasa imebadili mfumo wa ulipaji ada ya shilingi 1000 kila mwezi kwa wahudumu wa tuktuk kwenye kaunti hiyo.
Mfumo huo unalenga kupunguza msongamano na kukabiliana na ufisadi miongoni mwa maafisa wa kaunti.
Wahudumu hao wanaitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuwapa muda zaidi ili kuhamia katika mfumo huo wakisema hawakushirikishwa kikamilifu na hakuna uhamasisho uliofanywa.
Wanasema hatua hiyo itawalazimu kulipia huduma hizo kwenye sehemu za mitandao hali ambayo itawaathiri zaidi baadhi yao.
Kwa upande wake Job Tumbo ambaye ni mkuu wa wafanyikazi katika kaunti hiyo amesema mfumo huo utasaidia kuboresha huduma na kuwataka kushirikiana na serikali ya kaunti hiyo ili kufanikisha mfumo huo.
MFUMO WA ULIPAJI ADA WABADILISHWA KAUNTI YA MOMBASA

