GAVANA WA KAUNTI YA TAITA TAVETA ANDREW MWADIME AAHIDI KUIMARISHA MIUNDO MSINGI KAUNTI HIYO.

Gavana wa Kaunti ya Taita taveta Andrew Mwadime amewahakikishia wakaazi kuwa serikali yake, itafanya kila jitihada kuboresha kaunti hiyo na kuifanya Kuwa miongoni mwa kaunti bora ZAIDI nchini.

Akihutubia bunge la kaunti hiyo kwa mara ya kwanza, tangu achukue hatamu ya uongozi Mwadime amelitaka bunge hilo, kushirikiana vilivyo na serikali yake ili kutoa suluhu kwa changamoto zinazowakabili wakaazi kwa sasa.

Mwadime  amesema tayari amelipa wafanyikazi mishahara yao ya  miezi miwili, waliyokuwa wakidai ishara kuwa serikali yake itatoa kaunti ya Taita taveta kutoka kwa orodha ya kaunti za mwisho kimaendeleo na kuifanya kuwa kielelezo nchini.

Aidha, ameratibisha sekta ya elimu, ajira na afya kama nguzo kuu za kushughulikiwa kwa dharura.