SHIRIKISHO LA KENAFF LAWAALIKA WAKULIMA KATIKA MAOENYESHO YA KILIMO KAUNTI YA KILIFI.

Wakilima pamoja na wakaazi wa kaunti ya Kilifi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kupokeza mafunzo kuhusiana na masuala ya kilimo, katika maoenyesho ya kilimo yatakayofanyika katika uwanja wa Alaskan hapa mjini Malindi.

Akitaoa taarifa hizo kwa wanahabari mwenyekiti wa shirikisho la wakulima kitaifa la KENAFAA Bi Gertrude Bahati, amesema kuwa wakulima wanapaswa kuhamasishwa kuhisiana na teknolojia mpya ya kilimo, ili kuboresha mazao na hata mapato yao kwa jumla.

Ameongeza kuwa katika maonyesho hayo, wakulima watapata ufahamu mkubwa zaidi kuhusiana na jinsi wanavyoweza kutekeleza kilomo biashara.

Kwa upande wake naibu mwenyekiti wa shirikisho hilo Jonathan Kazungu Bugo, amesema kuwa wakulima wadogo wadogo huchangia pakubwa katika uchumi na hata upatikanaji wa vyakula asili sokoni kote ulimwengine.