SERERIKALI YA KAUNTI YA KWALE YAAHIDI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

Serikali ya Kaunti ya Kwale imeahidi kuipa kipaumbele sekta ya afya ili kuhakikisha kila mkaazi anapata huduma bora za matibabu.

Akiongea katika wadi ya Macknon Road katika shughuli ya kutoa hundi ya basari kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Gavana wa kaunti hiyo ya Kwale Fatuma Achani amesema kuwa tayari mikakati imeidhinishwa kuimarisha sekta ya afya kwenye kaunti hiyo  

Achani hata hivyo amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Kwale kuwa mstari wa mbele kuripoti visa vya utepetevu miongoni mwa wahudumu wa afya.

Achana amefichua kuwa serikali yake ina mipango ya kuongeza mgao wa fedha za basari kwa minajili ya kukidhi ongezeko la idadi kubwa ya wanafunzi watakaonufaika na mpango huo.

Wakaazi wa eneo hilo wameupokea vyema mpango huo wakieleza kuwa utawasaidia katika kupunguza mzigo wa kulipa karo.