Wakaazi wa Kilifi kusini kaunti ya Kilifi wamempongeza rais William Ruto kwa kumteua Aisha Jumwa kwenye baraza lake la mawaziri.
Wakaazi hao hasa kutoka eneo la Mtwapa wameeleza furaha yao kwa kuteuliwa kwa Jumwa wakiamini kuwa atamudu kudumisha utendakazi bora katika wizara hiyo.
Aidha wamempongeza rais Ruto kwa kuwateua wanawake wengi zaidi kwenye baraza lake la mawaziri wakisema kuwa ni ishara kubwa kuwa rais atamudu kutimiza ahadi zake alizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni zake.
Wakati uo huo wameeleza kunufaika pakubwa kama wakaazi wa kaunti ya Kilifi kutokana na swala kuwa spika wa bunge la seneti Ammason Jeffa Kingi na waziri mteule Aisha Jumwa wote ni wakaazi wa kaunti hii ya Kilifi.
Wamemtaka Jumwa kuendeleza ukakamavu wake licha ya pingamizi anazopata kutoka kwa wapinzani wake.

