Vijana ambao walisimamishwa kazi katika bandari ya Mombasa wametoa wito kwa rais William Kipchirchir Arap Ruto pamoja na washikadau katika mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini KPA kuwaregesha kazini.
Wakiongozwa na Hussein Khalid Hussein wamesema kuregeshwa kwa huduma za bandari kaunti ya Mombasa kutawawezesha vijana kupata nafasi za kazi na pia kuboresha uchumi wa kaunti hiyo na kanda ya pwani kwa jumla.
Kauli yao ambayo inajiri baada ya huduma hizo kuanza kuregeshwa bandarini humo amesema nafasi za kazi katika bandari ya Mombasa zinapaswa kupewa vijana kwanza akidai kila panapotokea nafasi za ajira vijana wamekuwa wakibaguliwa.

