GAVANA WA LAMU AMEAHIDI KUBORESHA KISIWA CHA LAMU

Serikali ya kaunti ya Lamu imeeleza kuwepo kwa mikakati ya kukabiliana na hali ya kutapakaa kwa vinyesi vya Punda katika baadhi ya miji ya kaunti hiyo.

Kulingana na Gavana wa kaunti hiyo Issa Abdalla Timamy wana mpango wa kutengeneza kiwanda kitakachobadilisha kinyesi hicho na kuwa makaa yanayoweza kutumika katika masuala ya upishi.

Gavana huyo amesema wananchi watalazimika kuzoa kinyesi na kukisafirisha hadi kwenye, kiwanda hicho.

Haya yanajiri baada ya wakaazi wengi wa kaunti hiyo, kulalamikia suala la ongezeko la kinyesi cha hayawani hao, katika mitaa iliyoko kaunti ya Lamu.