WANACHAMA WA PAA WAMPONGEZA AMASON KINGI

Wanachama wa chama cha PAA wamepongeza hatua ya kuchaguliwa kwa kinara wao Amason Jeffa Kingi kuwa spika wa bunge la seneti.

Wakiongozwa na mwanachama wao Hassan Albeity wanachama hao wamesema  hatua hiyo imedhihirisha wazi kuwa viongozi wa pwani wanatambuliwa katika ngazi ya kitaifa.

Albeity pia amesema Kingi anastahili kupata wadhifa huo kufuatia tajriba yake ya uongozi sawia na kiwango chake cha masomo.

Ni kauli iliyoungwa mkono na Harriet Mganda ambaye amesema kuchaguliwa kwa Kingi kuwa spika wa bunge la Seneti sio kwa manufaa yake tu bali ni kwa manufaa makubwa ya wakaazi wa Kilifi na wapwani kwa jumla.