Gavana wa kaunti ya Lamu Abdalah Issa Timamy, amesema kuwa sharti shughuli za kuwalipa fidia wavuvi katika kaunti ya Lamu litekelezwe kwa haki na uwazi.
Gavana huyo amesema wanafahamu kuwa wapo baadhi ya watu ambao sio wavuvi na tayari wameorodheshwa kupokea fedha hizo kutoka kwa serikali jambo ambalo amesema sio sahihi.
Akizungumza na wakaazi wa kaunti hiyo, kiongozi huyo amesema kuwa kama serikali ya kaunti, watakabidhi tume ya kukabiliana na ufisadi nchini EACC, jukumu la kuwachunguza baadhi ya wale ambao wameorodheshwa kupokea fidia hizo, iwapo ni wavuvi walio athirika na ujenzi wa bandari ya Lappset kaunti ya Lamu.
Aidha, amesisitiza kuwa iwapo haki itatendeka, wavuvi hao sasa watapata nafasi ya kujiendeleza katika shughuli zao.

