WATALI 15 WAHUSIKA KWENYE AJALI ENEO LA NYALI KAUNTI YA MOMBASA.

Zaidi ya watalii 15 wanauguza majeraha tofauti baada ya basi walilokuwa wameabiri kuhusika kwenye ajali katika eneo la Nyali kaunti ya Mombasa.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, basi hilo lililokuwa limetoka katika eneo la lights lilipoteza mwelekeo na kugonga lori sehemu ya nyuma na kisha kugonga nguzo ya umeme.

Majeruhi wamefikishwa hospitalini kwa matibabu.

Polisi walifika katika eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na chanzo cha ajali hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *