WANAHARAKATI KAUNTI YA KWALE WALALAMIKIA ONGEZEKO LA MAGENGE YA KIUHALIFU.

Wazazi eneo la Kinango kaunti ya Kwale wametakiwa kuchunguza mienendo ya wanao mitaani, ili kuwasaidia kuepuka kujiunga na makundi ya kiuhalifu.

Haya ni kwa mujibu wa mwanaharakati wa kijamii katika eneo hilo Juma Banda, ambaye amelalamikia ongezeko la idadi ya makundi ya kiuhalifu katika eneo hilo.

Banda amesema kuwa hatua hiyo, imeendelea kutishia usalama wa wananchi na huenda kukashuhudiwa athari nyingi zaidi iwapo jamii haitachukua hatua za haraka kuthibiti suala hilo.

Banda amependekeza mashirika ya kijamii nchini, kujitokeza na kuwapatia vijana mafunzo ambayo, yatawasaidia katika kuanzisha biashara na uwekezaji, ili kujiepusha na suala la kujiunga na makundi ya kiuhalifu eneo hilo la Kinango kaunti ya Kwale.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *