WALEMAVU KAUNTI YA KILIFI WAWASILISHA KESI KATIKA MAHAKAMA YA MALINDI.

Watu wenye uatilifu eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi wamewasilika kesi katika mahakama ya Malindi, kwa madai ya kukosa kuwakilishwa kikamilifu katika bunge jipya la kaunti ya Kilifi.

Akidhibitisha hilo mwanaharakati wa kutetea haki za walemavu eneo hili Willy Mwangi, amesema kuwa licha ya walemavu kusajiwa katika vyama mbali mbali ya kitaifa eneo hili, bado walikosa kupewa nafasi katika bunge hilo.

Akizungumza na mwanahabari wetu katika mahojiano ya kipekee, Mwangi amesema kuwa licha ya wao kulalamikia suala hilo katika afisi za uongozi wa kaunti hii na hata kufanya maandamano katika majengo ya bunge hilo, wakati wa kuapishwa kwa viongozi wa bunge la kaunti hii, hakuna hatua zozote zimechukuliwa.

Amesema kuwa walemavu wanapaswa kupewa kipaumbele, katika uteuzi wa wawakilishi wadi kwenye bunge la kaunti, kwa mujibu wa sheria za taifa hili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *