SERIKALI YA KITAIFA YATAKIWA KUKARABATI BARABARA ENEO LA GAMBA KAUNTI YA TANA RIVER.

Wizara ya uchukuzi nchini imetakiwa kukarabati barabara katika eneo la Gamba kaunti ya Tana River, msimu huu ambapo kuna shuhudiwa kiangazi eneo hilo.

Kwa mujibu wa meneja wa bandari ya Lamu, mhandisi Vincent Sidai, ujenzi wa barabara hiyo unaweza kufanikishwa kwa urahisi, msimu huu wa kiangazi, kabla ya mvua kuanza kushuhudiwa.

Sidai ameelezea wasiwasi wa madereva wanaobeba mizigo kutoka bandari ya Lamu, kukabiliwa na changamoto za usafiri watakapo tumia barabara hiyo msimu mvua itakapoanza kunya.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na wananchi wanaotumia barabara hiyo, ambao wameilaumu serikali kuu, kwa kukosa kuwajibikia ujenzi wa barabara hiyo eneo la Gamba.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *