Wizara ya elimu nchini imewahakikishia walimu wakuu katika shule za upili za umma, kuwa watapokea deni lao la shilingi bilioni 14, za muhula huu wa kwanza wiki hii.
Waziri wa elimu Julius Ogamba Migosi, amesema kuwa fedha hizo ni asilimia 25 ya jumla ya pesa ambazo, taasisi hizo zilitarajiwa kupokea katika muhula huu wa kwanza.
Akithitisha hilo, Migosi amesema kuwa majukumu mengi ya serikali, ndiyo chanzo cha kucheleweshwa kwa fedha hizo kwa shule za upili nchini muhula huu.
Aidha, amewataka walimu kutokuwa na wasiwasi wa kufanikishwa kwa mipango ya kuendesha shughuli za elimu nchini, kwani watapokea fedha hizo juma hili.

