Mradi wa ReSea Kuimarisha Maisha ya Jamii za Pwani

Wamama kaunti ya Kilifi wametakiwa kujihusisha na shughuli za utunzi wa mazingira pamoja na Uchumi wa rasilimali za maziwa na bahari nchini, ili kujiinua kiuchumi na kuepuka dhulma za kijinsia kwenye jamii.

Kwa mujibu wa afisa mkuu kwenye idara ya jinsia, utamaduni na vijana hapa kaunti ya Kilifi Agneta Karembo, ni kuwa ukosefu wa uwezo mzuri wa kifedha kwa baadhi ya akina mama, kuwa chanzo cha wao kutoripoti visa vya dhulma za kijinsia wanavyotekelezwa majumbani mwao.

Akizungumza kwenye hafla ya hafla iliyo andaliwa na shirika la Groots Kenya ili kuwasherehekea akina mama wanaofanyakazi kwenye sekta ya utunzi wa mazingira kaunti ya Kilifi, Karembo amepongeza miradi inayotekelezwa na shirika hilo ili kuwakwamua akina mama kutoka kwa hali ya umasikini akisema kuwa itasaidia pakubwa kwenye vita dhidi ya dhulma za wanawake mashinani.

Kwa upande wake afisa kwenye shirika hilo Peter Mathengi, ameelezea kuwa jumla ya makundi 28 yamenufaika na mradi huo hapa kaunti ya Kilifi na kwa sasa wanaendeleza mpango wa kuongeza thamani ya taka wanazo kusanya ili kuhakikisha kuwa wanapata fedha za kuwasiaida baada ya kuziuza.

Aidha mmoja wanawake ambao wamenufaika na mradi huo kwa jina Alice Katiwa, amewasisitiza akina mama kuwafunza wanao msimu huu wa likizo kuhusiana na namna ya kuhifadhi maji yaliyo tumika kwa shughuli mbali mbali ili yaweze kutumika tena kuendeleza kilimo nyunyizi.

Mradi wa Regenerative Seascapes Project for People, Climate and Nature (ReSea) unalenga kuimarisha ustahimilivu wa kimwili na kiuchumi kwa wanawake, wanaume, na vijana wanaoishi katika jamii za pwani nchini Kenya, Tanzania, Msumbiji, Comoro, na Madagascar. Nchini Kenya, mradi huu unatekelezwa katika maeneo ya Kilifi Kaskazini, Malindi, na Magarini katika Kaunti ya Kilifi. Asante. Mradi huu unafadhiliwa na serikali ya Canada.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *