RAIS WILLIAM RUTO AENDELEZA AHADI ZAKE KWA WAKAAZI WA PWANI.

Rais William Ruto wamehakikishia wakaazi wa Pwani kuwa watashuhudia miradi mingi ya maendeleo itakayo endelezwa na serikali yake.

Akizungumza katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa, kwenye ziara yake hapa Pwani, Ruto amesema kuwa kwa mda mrefu, kaunti za Ukanda huu zimeendelea kusalia nyuma kimaendeleo, kwani zimekuwa zikitengwa na serikali kuu.

Akihutubia umma, amewataka wakaazi wa eneo la Pwani, kuunga mkono serikali ya Kenya kwanza, ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kunufaika na miradi ya maendeleo kitaifa.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Mombasa, Abdulswamaad Shariff Nassir amemsuta aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, kwa madai ya kuendekeza ukabila.

Mbunge eneo hilo la Likoni, Mishi Mboko amempongeza rais William Ruto kwa kuchukua hatua ya kuungana na Raila Odinga, katika kuhudumia wakenya.

Aidha, Rais William Ruto anatarajiwa kuzuru maeneo bunge ya Matuga, Msambweni na LungaLunga katika kaunti ya Kwale hii leo, ambapo atazindua miradi mbali mbali ya umeme wa Last Mile Conectivity, Chumba cha upasuaji, mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu na ugavi wa hati miliki za ardhi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *