Huenda rais William Ruto sasa akaungana kisiasa na aliyekuwa kinara wa Odm Raila Odinga.
Haya ni kutokana na kauli ya Raila katika ikulu ya rais kaunti ya Mombasa, ambapo kiongozi huyo aliahidi kutoa taarifa, kuhusiana na muelekeo kwa kisiasa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya kwanza.
Kauli yake iliungwa mkono na rais William Ruto, ambaye alisema kuwa kuna haja ya wawili hao sasa, kuangazia zaidi masuala ya ushirikiano na mshikamano katikati ujenzi wa taifa hili.
Rais Ruto aidha ametetea ushirikiano wake na Raila, akisema kuwa umechangiwa pakubwa na umoja ambao, anadai umeshuhudiwa kati ya wakenya, hasa wakati huu ambapo Odinga, amekuwa akiwania wadhifa wa mwenyekiti wa tume ya mataifa ya Afrika AUC, kauli yake ikiungwa mkono na naibu wake Profesa Kithure Kindiki.

