JAMII YA MIJIKENDA YAANZA MIKAKATI YA KUFUNZA VIJANA TAMADUNI HIYO.

Huenda visa vya mauaji ya wazee kwa tuhma ya uchawi huko Garashi eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi vikapungua kwa kiwango kikubwa, baada ya kuzinduliwa kwa kituo cha kitamaduni, kitakachotoa mafunzo ya mila na desturi za kimijikenda.

Mwanzilishi wa kituo hicho Alex Katana, amefichua kuwa baadhi ya vijana wa kizazi cha sasa, wamekuwa wakitekeleza visa hivyo kutokana na suala la wao kupotoka kimaadili.

Katana amesisitiza kuwa kituo hicho, kilichoko eneo la Bore, kitazingatia zaidi kutoa mafunzo kwa vijana, ili kuhakikisha kuwa wanakumbatia mila na tamaduni za jamii ya Mjikenda.

Kwa upande wake kiongozi wa wachungaji katika eneo la Garashi, Emmanuel Kikami, amewataka wachungaji kukoma kuhusisha vituo vya kuhifadhi mila na maswala ya ushirikiana na badala yake kushirikiana na wamiliki wa vituo hivyo katika kuelimisha jamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *