JAMII KAUNTI YA MOMBASA YATAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA VITA DHIDI YA UTUMIZI WA MIHADARATI.

Gavana wa kaunti ya Mombasa, Abdulswamad Sharif Nassir ametoa wito kwa viongozi kwenye jamii kaunti hiyo, kushirikiana ili kukuza talanta za vijana.

Nassir amesema katika kufanya hivyo, watasaidia pakubwa vijana wengi ambao hupotoka kimaadili kwenye jamii na kujihusisha na utumizi wa mihadarati.

GAVANA huyo aidha amewashauri vijana, kutohusisha talanta na utumizi wa mihadarati kwani itaathiri afya zao.

Aidha, amesisitiza haja ya jamii kuwashauri vijana kutojihusisha na uovu wa aina yeyeto kwenye jamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *