JAMII ENEO LA RABAI KAUNTI YA KILIFI ZAKABILIWA NA BAA LA NJAA.

Idadi kubwa ya wananchi katika vijiji vya eneo bunge la Rabai hapa kaunti ya Kilifi, wameendelea kukabiliwa na changamoto kuu ya ukame.

Kulingana na kamishna wa eneo bunge hilo Joseph Lenkari, wananchi hao hawajakuwa wakipokea mvua za kuwasaidia kupata mazao bora shambani kwa takriban miaka miwili sasa.

Akizungumza katika eneo hilo, Lenkari amesema kuwa idadi kubwa ya watoto katika maeneo ya Kanyumbuni, Kazameni, Moyo na Ngamani, wamekuwa wakivumilia makali ya njaa, kutokana na ukosefu wa chakula unaosababishwa na kiangazi kikali, kinacho shuhudiwa eneo hilo.

Hata hivyo amewaonya wanajamii katika kijiji cha Mwawesa, dhidi ya kuwaua wazee kwa tuhuma za uchawi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *