CHAMA CHA DCP KUUNGA MKONO WAGOMBEA WA VYAMA MBADALA KATIKA MUUNGANO WA UPINZANI.

Chama cha DCP kimeridhia kuunga mkono viongozi wa vyama tofauti katika mrengo upinzani, kwenye changuzi ndogo zinazo tayariwa kufanyika katika maeneo tofauti ya taifa, mwezi novemba mwaka huu wa 2025.

Kinara wa chama hicho Rigathi Gachagua, amesema kuwa maeneo ambayo chama hicho kitaunga mkono vyama vingine, ni pamoja na Mbeere Kaskazini kaunti ya Embu, wadi ya Mumbuni kaunti ya Machakos, wadi za Kabuchai na Chwele kaunti ya Bungoma.

Katika taarifa yake kwa wanahabari, amesema kuwa uamuzi huo ni kutokana na nia ya muungano wa upinzani, kuweka msingi wa jinsi watakavyo mbandua rais William Ruto mamlakani mwaka 2027.

Hata hivyo chama hicho kimeelezea kutofurahishwa na hali ya usalama kwa sasa katika kaunti ya Mandera, baada ya wananchi na viongozi wa katika kaunti hiyo, kulalamikia suala la uwepo wa wanajeshi wa Juba Land kaunti hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *