Baadhi ya vijana wa kizazi cha Gen Z kupitia mtandao wa Tiktok, wametishia kuchangisha pesa mtandaoni na kujenga hospitali ya kisasa, itakayo toa huduma muhimu za matibabu na za bure kwa wakenya wanao hangaika.
Kulingana na vijana hao, hatua hiyo itawawezesha kusaidia wakenya wanaokabiliwa na changamoto za kupata huduma za matibabu kitaifa.
Hesabu za vijana hao ni kama zifuatavyo.
Kenya ina takriban vijana milioni 18 na iwapo kila kijana atajitolea kuchanga shilingi mia moja, basi watafanikiwa kupata shilingi bilioni 1.8, na iwapo mchango huo utaendelezwa kwa siku tatu, basi watafanikiwa kupata shilingi bilioni 5.4.
Ikumbukwe kwamba gharama ya ujenzi wa baadhi ya hospitali kuu humu nchini, imekuwa ikiratibiwa kuwa kati ya shilingi bilioni 1 hadi 2.