IDARA YA POLISI YAHAKIKISHIA WAKENYA UHURU NA HAKI KATIKA ZOEZI LA USAJILI WA MAKURUTU.

Idara ya polisi nchini imewahakikishia wakenya kuwa zoezi la kuwasajili makurutu elfu kumi kitaifa litakuwa huru na haki.

Inspekta mkuu wa Polisi Douglas Kanja, amesema kuwa hakuna mtu yeyote anastahili kulipishwa ada zozote, ili kupata nafasi ya kujiunga na kikosi cha maafisa wa polisi nchini NPS.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kanja amesema kuwa wanalenga kuhakikisha kuwa zoezi hilo, lina endeshwa kwa uadilifu wa hali ya juu zaidi.

Kanja amewataka wakenya kuripoti visa vyovyote vya ulaghali kwa idara ya polisi wakati shughuli hizo, zikiendelezwa kote nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *