WANAKANDARASI WAONYWA DHIDI YA ULEGEVU KATIKA UTEKELEZWAJI WA MIRADI YA SERIKALI KUU.

Wanakandarasi nchini wameonywa dhidi ya kutokamilisha miradi ya serikali ya kitaifa kwa wakati.

Waziri wa madini na uchumi wa rasilimali ya bahari na maziwa nchini Ali Hassan Joho, amesema kuwa idadi kubwa ya miradi inayo anzishwa na serikali, imekuwa ikikawia kukamilika, pasi na sababu zozote za kimsingi.

Akizungumza katika kaunti ya Kwale, kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya tofauti ikiwemo ujenzi wa ukuta baharini, eneo la Gazi katika wadi ya Kinondo, Joho amewataka wambunge na wawakilishi wadi, kuhakikisha kuwa wanakagua utekelezwaji wa miradi ya serikali kuu mara kwa mara.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kwale, Fatuma Achani amepongeza utekelezwaji wa miradi ya serikali kuu katika kaunti hiyo huku akielezea kuwa na imani itawafadi wananchi pakubwa.